*Aprili 12, 1984: Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Tanzania
anafariki dunia katika ajali ya gari katika barabara kuu ya Dodoma-Dar
es Salaam, kando tu ya eneo la Dakawa, Morogoro. Ni moja ya misiba
mikubwa zaidi kuikumba Tanzania.
*Aprili 12, 1988: Chuo Kikuu cha Harvard ambacho kinaheshimika kuliko
vyote duniani, kinasajili kisheria uvumbuzi wa panya aliyetengenezwa
bila kuzaliwa (genetically engineered) katika moja ya maabara za Chuo
Kikuu hicho.
*Aprili 12, 1987: Texaco, moja ya makampuni makubwa zaidi ya mafuta
wakati wake, inaiomba mahakama iitangaze imefilisika, Hii ni muda
mfupi baada ya kuambiwa ilipe fidia kubwa kuliko zote duniani kwa
wakati huo katika kesi ya kusisimua ambapo Texaco ilishtakiwa na
kampuni ndogo ya mafuta ya Pennzoil iliyotetewa na mwanasheria mahiri
na tajiri zaidi duniani, Joe Jamail wa Houston, Texas.
*Aprili 12, 1947: Tom Clancy, mtunzi mashuhuri wa vitabu duniani anazaliwa.
*Aprili 12, 1903: Jan Tinbergen, Mchumi mashuhuri wa Uholanzi na
mshindi wa tuzo ya Uchumi ya Nobel ya mwaka 1969, anazaliwa.
No comments:
Post a Comment