Monday, February 27, 2012

APRILI 6 MATUKIO MUHIMU KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

• Aprili 6, 1985: Katiba ya nchi ya Sudan inasimamishwa baada ya
kufanyika mapinduzi ya kijeshi yanayoongozwa na Jenerali Swarreddahab.
• Aprili 6, 1917: Marekani inaingia rasmi katika Vita vya Kwanza vya Dunia.
• Aprili 6, 1992: Majeshi ya Serbia yanauteka mji maarufu wa Sarajevo.
• Aprili 6, 1991: Diego Maradona, mwanasoka maarufu wa Argentina
aliyewahi kuwa mwanasoka bora duniani, anasimamishwa kucheza ligi ya
Italia baada ya kubainika kutumia madawa haramu ya Cocaine.
• Aprili 6, 1972: Misri inavunja uhusiano wa Kibalozi na nchi ya Jordan.
• Aprili 6, 1964: Misri inarejesha uhusiano wa kibalozi na Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment