*Mei 23, 1988: Mwalimu Nyerere anaeleza katika mkutano na waandishi wa
habari kuwa uamuzi wowote wa kufuta Azimio la Arusha nchini utaleta
machafuko na maandamano makubwa kama yale yaliyofanyika wakati wa
kuunga mkono Azimio hilo mwaka 1967.
*Mei 23, 1993: Rashid Mfaume Kawawa anatangaza kustaafu kutoka
utumishi wa Umma nchini Tanzania.
*Mei 23, 1945: Winston Churchill anajiuzulu U-Waziri Mkuu wa Uingereza.
*Mei 23, 1989: Angela Visser, 22, wa Uholanzi anashinda tuzo la mrembo
bora zaidi duniani (Miss Universe)
*Mei 23,1430: Joan wa Arc, mwanamke anayetajwa kuwa mmoja wa waliokuwa
shujaa na jasiri zaidi katika historia, anakamatwa na kuuzwa kwa
Waingereza.
*Mei 23,1974: Jewel Kilcher, mwanamuziki maarufu aliyeuza zaidi ya
nakala milioni 27 za albamu zake, anazaliwa. Hucheza sinema pia.
*Mei 23, 1934: Wallace Carothers anatengeza nailoni ya kwanza kabisa duniani.
*Mei 23, 1928: Watu 22 wanakufa katika bomu ndani ya ubalozi wa
Italia jijini Buenos Aires, Argentina.
*Mei 23,1978: Silvia Colloca, mcheza sinema wa kike wa Italia anazaliwa.
No comments:
Post a Comment