*Aprili 4, 1952: Sir John Graham Gray anatangaza kustaafu wadhifa wa
Jaji Mkuu wa Zanzibar.
*Aprili 4, 2008: John Mndolwa, Mhariri Mratibu wa Habari ITV anafariki dunia.
*Aprili 4,1949: Mkataba wa Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya
Magharibi (NATO) unasainiwa jijini Washington D.C., Marekani.
*Aprili 4,1960: Senegal inapata uhuru kutoka kwa Ufaransa.
*Aprili 4,1969: Denton Cooley, daktari bingwa wa upasuaji mioyo kutoka
Houston, Texas, Marekani anafanikisha oparesheni inayowezesha kuwekwa
kwa moyo wa kwanza bandia katika binadamu.
*Aprili 4,1972: Mtambo wa kwanza duniani wa umeme uendeshwao kwa nguvu
za taka unaanza kazi.
*Aprili 4, 1823 : Karl Wilhelm Siemens, mvumbuzi wa utandazaji nyaya
chini ya bahari anazaliwa.
*Aprili 4,1994: Netscape Communications, kampuni ya mwanzo kubwa
kufanikisha utafutwaji wa taarifa katika mtandao wa kompyuta wa
internet inazaliwa ikaanza kwanza na jina la Mosaic Communications.
Baadaye ilizidiwa umaarufu na teknolojia ya utafutaji taarifa ya
Intenet Explorer iliyotolewa na kampuni ya Microsoft ya bilionea Bill
Gates.
*Aprili 4,1989: Kareem Abdul-Jabbar, mcheza mpira wa vikapu mahiri
zadi duniani wakati wake, anacheza mchezo wake wa mwisho jijini
Seattle, Marekani.
*Aprili 4,1978: Irene Skliva, mrembo bora zaidi duniani (Miss World)
kwa mwaka 1996, anazaliwa huko Athens, Ugiriki.
No comments:
Post a Comment