Friday, February 24, 2012

JUNI 11 KATIKA HISTORIA (JUNE 11 HISTORY IN KISWAHILI)

*Juni 11, 1979: Mwalimu Nyerere anaelezakufurahishwa na tamko la rais
Moi wa Kenya kuitisha kikao cha viongozi wa Afrika Mashariki kujadili
namna ya kuijenga Uganda iliyoharibika kutokana na utawala wa nduli
Amin na athari za Vita vya Kagera.
*Juni 11, 1998: Basil Mramba, Waziri wa Fedha Tanzania, anawasilisha
bajeti ya serikali bungeni ambapo kwa mwaka 1998/1999 Tanzania
ingetumia shilingi milioni 1, 007, 786 ambapo kati ya hizo milioni
264.465 ni katika mipango ya maendeleo.
*Juni 11, 1994: Moshood Abiola anakuwa Rais wa Nigeria.
*Juni 11, 1982: Vita vya Israel na Syria vinamalizika huko Lebanon.
*Juni 11, 1987: Margaret Thatcher anakuwa Waziri Mkuu anayevunja
rekodi ya miaka 160 ya Waziri Mkuu aliyekuwa madarakani kushinda awamu
ya tatu ya kuongoza Uingereza.

No comments:

Post a Comment