Juni 10
*Juni 10, 1967: Rais Nyerere anafanya mabadiliko katika baraza la
mawaziri kwa kuwateua mawaziri wadogo kadhaa akiwemo Bibi Lucy Selina
lameck anayekuwa Naibu Waziri wa Afya. Mawaziri kamili ni pamoja na
akina Oscar Kambona na Peter Kisumo.
*Juni 10, 1999: Daniel Yona, waziri wa fedha, anatangaza bajeti ambapo
kima cha chini kinapanda kutoka 2, 000 hadi 10,000/= na kodi katika
matrekta zinaondolewa.
*Juni 10, 1975: Tume ya Rockefeller inatoa ripoti ya kutisha pale
inapoeleza kuwa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lina mafaili laki
tatu (300,000) juu ya Wamarekani ambayo yalitengenezwa kinyume cha
sheria.
*Juni 10, 1985: Coca Cola inatangaza kuanza kutumia tena formula
(kanuni ya utengenezaji) ya kinywaji hicho ya miaka 99.
*Juni 10, 1988: Mbio za baskeli zinazowakutanisha waendesha baiskeli
wengi zaidi katika historia zinafanyika ambapo watu 31,678 wanashiriki
huko London, Uingereza.
*Juni 10,1981: Joseph Doherty, kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha
IRA, anatoroka kutoka katika jela.
*Juni 10,1981: Sebastian Coe wa Uingereza anaweka rekodi ya kukimbia
mita 800 kwa dakika 1 sekunde 41 nukta 73.
*Juni 10,1961: Maxi Priest, mwanamuziki maarufu wa Reggae, anazaliwa
huko Jamaica.
No comments:
Post a Comment