*Kesi ya Uhaini inasikilizwa tena na Jaji Mkuu nassor Mnzavas. Katika
kesi hiyo watuhumiwa kadhaa akiwemo Hatty MacGhee, Uncle Tom
Rugangira, George Banyikwa na wengineo walituhumiwa kutaka kuipindua
serikali na kumuua Mwalimu Nyerere aliyekiwa Rais wakati huo.
*Machi 26, 1983: Hali ya msongamano wa maiti katika chumba cha
kuhifadhia maiti muhimbili inaelezwa kuwa ya kutisha.
*Machi 26, 1976: Larry Page, moja wa waanzilishi wa wawili wa kampuni
ya Google (injini ya utafutaji taarifa katika intaneti) anazaliwa. Kwa
sasa ni mmoja wa mabilionea wakubwa zaidi duniani.
*Machi 26, 1944: Diana Ross, mwanamuziki maarufu wa kike mweusi wa
Marekani anazaliwa.
*Machi 26, 1863: Henry Royce, bilionea aliyeanzisha kampuni ya magari
ya kifahari ya Rolls-Royce anazaliwa.
**Machi 26, 1985: Keira Knightley, mcheza sinema maarufu wa kike wa
marekani anazaliwa.
*Machi 26, 1930: Jaji wa kwanza mwanamke katika mahakama ya juu zaidi
Marekani na mmoja wa wanawake wanaoheshimika sana katika taaluma ya
sheria duniani kote anazaliwa.
*Machi 26, 1913: Paul Erdos, mwenahisabati maarufu sana duniani anazaliwa.
No comments:
Post a Comment