*Juni 14, 1878: Alexander Mackay, mpelelezi kutoka Uingereza,
anawasili katika kisiwa cha Ukerewe ili kuchunguza kifo cha mzungu
O’Neall aliyeuawa kwa amri ya mfalme Lukonge wa Ukerewe baada ya
mzungu huyo kuua Wakerewe 30 na kujeruhi wengi kwa bunduki yake.
*Juni 14, 1958: Nelson Mandela anamuoa Winnie Mandela.
*Juni 14, 1974: Wizara mbalimbali zinaanza kuwasilisha bajeti zao
bungeni baada ya Waziri wa Fedha Cleopa Msuya kuwasilisha bajeti ya
serikali ya 1974/75.
*Juni 14, 1942: Anne Frank mwanamke Myahudi aliyeandika diary (kitabu
cha kuandikia kumbukumbu za kila siku) maarufu zaidi duniani (kuhusu
mateso ya wayahudi wakati wa U-Nazi wa Ujerumani), anaanza kuanza
kuandika kumbukumbu zake hizo.
*Juni 14, 1989: Malkia Elizabeth II wa Uingereza anampa Rais Ronald
Reagan wa Marekani heshima ya juu zaidi kutolewa na nchi hiyo
(knighting) kwa mtu. Sasa Reagan anakuwa Sir Ronald Reagan.
1985: Ndege ya TWA Flight 847 inatekwa nyara na Waislamu wenye msimamo
mkali wa Kishia.
1972: Watu 117 wanakufa katika kimbunga aina ya Agnes.
No comments:
Post a Comment