Monday, February 27, 2012

MEI 3 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

Mei 3 historia
*Mei 3, 1965: Halmashauri Kuu za Vyama vya TANU (Tanzania Bara) na ASP
(Tanzania Visiwani) zinakubaliana na rasimu ya Kuifanya Tanzania kuwa
na Katiba ya Chama Kimoja cha Siasa.
*Mei 3, 1987: Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania anamueleza Waziri wa
Mambo ya Nje wa Burundi anayeitembea Tanzania, Edgar Nkuringoima kuwa
Tanzania ina ushahidi kuwa kuna raia wa Burundi zaidi ya 30,000
wanaoishi nchini Tanzania isivyo halali.
*Mei 3,1997: Garry Kasparov, bingwa mahiri wa mchezo wa Chess duniani
wakati wake anapambanishwa kucheza mchezo huo wa kutumia akili nyingi
na programu ya kompyuta kutoka IBM, Deep Blu. Kompyuta inashinda kwa
tabu.
*Mei 3,1469: Niccolo Machiaveli, mwanafalsafa mashuhuri wa siasa na
utawala kutoka Italia na mtunzi wa kitabu maarufu cha ‘Prince’,
anazaliwa.
*Mei 3,1898: Golda Meir, Waziri Mkuu wa nne wa Israel (na wa kwanza
mwanamke) kati ya (1969-1974) anazaliwa.
*Mei 3,1892: George Thompson aliyeshinda tuzo ya Nobel mwaka 1937 kwa
utafiti wa tabia za kifizikia za elektroni, anazaliwa.
*Mei 3,1845: watu zaidi ya 1, 600 wanakufa kwa moto katika ukumbi
mmoja mkubwa wa burudani huko China.

No comments:

Post a Comment