* Mei 2, 1988: Meli ya M.V Serengeti yenye uzito wa tani 500 na yenye
kubeba abiria 350na mizigo tani 350 inazinduliwa kwa safari katika
Ziwa Victoria na Rais Ali Hassan mwinyi kwa ufadhili wa Shirika la
Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Denmark, DANIDA.
*Mei 2, 1974: Kampuni ya Dar es Salaam Motor Transport (DMT) inavunjwa
na badala yake zinazaliwa kampuni za UDA (Usafiri Dar es Salaam) na
Shirika la Mabasi ya taifa (KAMATA)
* Mei 2,1963: Mikoa ya Kilimanjaro, Ruvuma, Mara na Shinyanga inaanzishwa rasmi.
*Mei 2,1974: Kitengo cha Elimu ya wafanyaki kinaundwa ndani ya Wizara
ya kazi na Ustawi wa Jamii.
*Mei 2,1949: Arthur Miller, mtunzi maarufu wa fasihi anashinda tuzo ya
uandishi ya Pulitizer kwa utunzi wake maarufu, Death of the Salesman,
kitabu kilichotumika kufundishia fasihi kote duniani, ikiwemo
Tanzania.
*Mei 2, 1946: Ghasia katika gereza la Alcatraz, Marekani ambalo ni
moja ya yale yuanayolindwa zaidi duniani, zinaziuka na watu 5
wanakufa.
*Mei 2,1945: Vita vya Pili Vya Ulimwengu vinazidi kukaribia ukingoni
baada ya majeshi ya NAZI ya Ujerumani ya Adolf Hitler kusalimu amri
huko Italia.
*Mei 2,1975: David Beckhan, mcheza soka mashuhuri wa Uingereza na mume
wa Posh Spice (kundi la muziki la Spice Girls) anazaliwa.
*Mei 2,1976: Ailleen Damiles, Miss Universe-Philippines/Miss
Photogenic 1996 anazaliwa.
No comments:
Post a Comment