*Mei 11, 1848: John Rebman kutoka Ujerumani anakuwa mzungu wa kwanza
kuuona Mlima Kilimanjaro kwa macho yake mwenyewe.
*Mei 11, 1989: Seif Shariff Hamad, Waziri Kiongozi wa zamani wa
Zanzibar anafkishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika
mkusanyiko wa kisiasa usio halali. Hakimu Ramsa Mbarouk Foum anaagizwa
asweke ndani na asafirishwe Wete, Pembe kujibu mashtaka huko.
*Mei 11,1993: watuhumiwa 49 wa kuchoma mabucha ya nguruwe jijini Dar
es Salaam wananyimwa dhamana na Hakimu Projestus Rugazia hata baada ya
mawakili wao Nasib Mselem, Musa Kwikima na Yusuf Mchora kueleza kuwa
sababu za kuwanyima dhamana zilizotolewa na mwendesha mashaka Mratibu
wa Polisi Leonard mashaka hazikuwa na nguvu za msingi kisheria.
*Mei 11, 1993: Garth Brooks anashinda tuzo ya mwanamuziki bora wa
mahadhi ya Country katika tamasha la 29 la muziki wa Country.
*Mei 11, 1985: Watu 40 wanakufa na wengine 150 kujeruhiwa vibaya
katika ajali ya moto katika uwanja wa soka wa jiji la Bradford,
Uingereza.
*Mei 11, 1984: Johan Cruiff, mwanasoka mashuhuri wa zamani wa uholanzi
aliyetamba katika kombe la dunia, anastaafu mchezo huo.
*Mei 11, 1978: Laetitia Casta, mwanamitindo mashuhuri na mcheza sinema
wa kike aliyepamba zaidi ya kurasa za magazeti 100 na matangazo ya
makampuni makubwa ya urembo anazaliwa.
*Mei 11, 1904: Salvador Dali, msanii mchoraji maarufu kutoka
Hispania, anazaliwa.
No comments:
Post a Comment