Tuesday, February 28, 2012

MARCH 9 EVENTS IN HISTORY (MACHI 9 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI)

Machi 9 historia
*Machi 9, 2005: Jakaya Kikwete, Waziri wa mambo ya Nje wakati huu
anasema kuwa angekuwa mpiga debe mkuu wa Rais Mkapa anayemaliza muda
wake kama katiba ya nchi ingeruhusu aongezewe muda wa kutawala.
*Machi 9, 2005: John Malecela, Makamu mwenyekiti CCM Malecela anakataa
kupeperusha bendera ya CCVM katika gari lake wakati wa zoezi la
kutafuta wadhamini kugombea urais mjini Mbeya
*Machi 9, 2005: Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM) alhaji Ahmed Mpeme
anatangaza kutogombea tena ubunge.
*Machi 9, 1983: Joshua Nkomo: Mwanasiasa wa upinzani wa Zimbabwe
anakimbilia uhamishoni Botswana.
*Machi 9, 1980: Mwanamuziki maarufu mweusi wa Marekani, Chingy (jina
halisi Howard Bailey, Jr) anazaliwa.
*Machi 9, 1791: George Hayward, mwanasayansi na daktari maarufu na wa
kwanza kutumia kemikali ya ganzi ya Ether wakati wa kufanya upasuaji,
anazaliwa.
*Machi 9, 1564: David Fabricius: Mwanasayansi na Mnajimu aliyevumbua
nyota yenye tabia ya kubadilika anazaliwa.

No comments:

Post a Comment