Monday, February 27, 2012

APRILI 30 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Aprili 30,1992: Muswada wa Mabadiliko ya Nane ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuruhusu mabadiliko kutoka mfumo wa Chama kimoja
cha Siasa kwenda Vyama vingi unawasilishwa Bungeni na John Samuel
Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wakati huu.
*Aprili 30, 1972: Mzalendo, Gazeti la Kiswahili la Kila Jumapili
linalomilikiwa na chama cha TANU (na baadaye CCM) linazaliwa.
*Aprili 30, 1982: Kirsten Dunst, mcheza filamu maarufu wa kike wa
Marekani aliyetamba na filamu ya Interview with the Vampire anazaliwa.
*Aprili 30, 1974: Rais Richard Nixon wa Marekani anasalimu amri kwa
kukubali kutolewa kwa rekodi kuhusiana na kashfa ya Watergate. Baadaye
alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo.
*Aprili 30, 1961: Fidel Castro, Waziri Mkuu wa Cuba wakati huu
anatunukiwa nishani ya amani ya Lenin.
*Aprili 30, 1900: Marekani inakitwaa kisiwa cha Hawaii na kukifanya jimbo lake.
*Aprili 30, 1859: Paul Morphy, mmoja wa binadamu mahiri zaidi katika
historia ya mchezo wa Chess duniani anastaafu.

No comments:

Post a Comment