Tuesday, February 28, 2012

MARCH 20 EVENTS IN HISTORY (MACHI 20 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI)

Machi 20
*Machi 20, 1978: Mahakama ya Rufaa ya Tanzania inampunguzia kifungo jela Thomas Zangira, Mtanzania wa kwanza na pekee kutiwa hatiani kwa kosa la kufanya ujasusi ndani ya Tanzania. Majaji Francis Nyalali, Robert Kisanga na Kahwa Lugakingira wanamuona na hatia Zangira lakini wanaeleza kuwa kifungo cha miaka 20 jela ni adhabu kubwa mno kwa mshtakiwa kama yeye kwa namna alivyotoa ushirikiano katika kesi hiyo na pia kutokuwepo ushahidi wa kuthibitisha kwa uhakika athari ambazo Tanzania ingezipata kwa kosa alilolifanya ambapo alidaiwa kutuma taarifa za kijasusi kwa Mzungu mmoja na jajusi wa kimataifa aitwaye John Wilson.
*Machi 20, 1727: Sir Issac Newton, mwanafikizia maarufu sana duniani, anafariki dunia akiwa na umri wa miaka 84
*Machi 20, 1977: Hayati Indira Gandhi anashindwa katika uchaguzi Mkuu wa India.
*Machi 20, 1969: John Lennon, mwanamuziki wa kundi maarufu la Beatle, anafunga ndoa na Yoko Ono.
*Machi 20, 1991: Michael Jackson anasaini mkataba mnono wa dola milioni 65 za Kimarekani ili kuirekodia kampuni ya Sony album sita.
*Machi 20, 1956: Tunisia inapata uhuru na kujikomboa kutoka ukoloni wa Wafaransa.
*Machi 20, 1815: Napoleon, mmoja wa majemedari maarufu zaidi waliopata kuishi anaingia jijini Paris na kuanza utawala wa siku 100, baada ya kuepuka kuuawa katika mapigano makali ya Elba.
*Machi 20, 1904: B. F. Skinner, mmoja wa Wanasaikolojia maarufu zaidi katika historia ya dunia, anazaliwa.
*Machi 20, 1986: Jacques Chirac anaunda serikali mpya ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment