Monday, February 27, 2012

MEI 19 MATUKIO KATIKA HISTORIA

*Mei 19, 1971: Sheikh Abed Amani Karume wa Zanzibar anatangaza katika
viwanja vya Maisera Selemani kuwa watu 19 huko Visiwani watauawa
hadharani kwa kupigwa risasi kwa vitendo vyao vya uhaini dhidi ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
*Mei 19, 1993: watu 132 wanakufa baada ya ndege aina ya Boeing
kuanguka katika mlima huko Medellin Colombia.
*Mei 19,1995: Balamurali Ambati (umri miaka 17 wakati huo) anakuwa
binadamu mdoo zaidi kuhitimu udaktari duniani na kupitia Chuo Kikuu na
Hospitali inayoheshimika katika tiba cha Mount Sinai.
*Mei 19,1967: Marekani inalipiga mabomu jiji la Hanoi wakati wa Vita
vya Vietnam.
*Mei 19,1960: Bunge la Ubelgiji linapitisha sheria ya kulazimisha hata
watu waliojiajiri wenyewe kuwa na siku ya mapumziko.
*Mei 19,1943: Utawala wa Ki-Nazi wa Ujerumani chini ya Adolf Hitler
unatangaza kuwa kuwa hakuna hata Myahudi mmoja anayeishi jiji la
Berlin kwa wakati huo baada ya kuwaua au kuwahamisha Wayahudi ambao
Hitler aliwachukia sana.
*Mei 19,1943: Sir Winton Churchill, Waziri Mkuu wa Uingereza
anatangaza kuisaidia Marekani katika Vita dhidi ya Japan, wakati wa
Vita vya Pili vya Dunia.
*Mei 19,1976: Kevin Garnett, mchezaji maarufu wa ligi ya Mpira wa
Kikapu ya marekani (NBA) anazaliwa..

No comments:

Post a Comment