*Aprili 5,1588: Thomas Hobbes, mwanafalsafa maarufu sana katika
historia anazaliwa huko Uingereza.
*Aprili 5,1937: Colin Powell, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani wa
zamani wa kwanza mweusi anazaliwa.
*Aprili 5,1984: Kareem Abdul-Jabbar, mmoja wa wacheza mpira wa vikapu
(Basket Ball) maarufu zaidi katika historia ya mchezo huo anavunja
rekodi kwa kufikisha pointi 31, 419 dhidi ya 31,419 zilizokuwa na
mwingine maarufu Wilt Chamberlain.
*Aprili 5,1939: Dikteta Adolf Hitler wa Ujerumani anasema vijana wote
ni lazima wajiunge na Umoja wa Vijana wa Chama chake cha NAZI.
*Aprili 5,1971: Krista Allen, mwanamke maarufu aliyetamba kama Billie
Reed katika tamthiliya ya 'Days of Our Lives' na pia kama Jenna Avid
katika tamthiliya ya 'Baywatch Hawaii' anazaliwa.
No comments:
Post a Comment