*Mei 16, 1986: Rajiv Gandhi, Waziri Mkuu wa India na mkewe Sonia
wanaondoka India kuja Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara ya kiserikali
ya siku mbili.
*Mei 16, 1964: Stephen Moshi anatangazwa kuwa Askofu wa kwanza wa
Kanisa la Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT)
*Mei 16, 1986: Megan Fox, mcheza sinema mashuhuri wa Marekani
anayetajwa na jarida la FHM kama mwanamke mwenye mvuto zaidi duniani,
anazaliwa.
*Mei 16, 1875: Watu 16, 000 wanakufa katika tetemeko la ardhi huko
Venezuela na Colombia.
*Mei 16, 1988: C. Everett Koop, Tabibu Mkuu wa Marekani anatangaza
kuwa kemikali maarufu kama nicotine zilizoko katika tumbaku na sigara
zinafanana na madawa ya kulevya hatari aina ya heroine katika tabia ya
kumfanya mtumiaji kuingia katika mtego wa kutoacha matumizi yake pale
anapoanza na kuzoea (maarufu kama kuwa ‘teja’)
*Mei 16, 1977: Muhammad Ali anamtwanga Alfredo Evangelist na kuwa
bingwa wa ndondi za uzito wa juu duniani kwa mara nyingine tena.
*Mei 16, 1941: Wajerumani chini ya diketa Hitler wanafanmya shambulio
kubwa la mwisho dhidi ya Uingereza wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
No comments:
Post a Comment