Monday, February 27, 2012

MEI 14 MATUKIO KATIKA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI KOTE

*Mei 14, 1973: Julie Manning anakuwa Jaji wa kwanza wa Mahakama Kuu
mwanamke nchini Tanzania.
* Mei 14, 1984: Marais Julius Nyerere wa Tanzania, Milton Obote wa
Uganad na Daniel Arap Moi wa Kenya wanakutana Asrusha kujadili namna
ya ushirikiano mpya baina yao baada ya kuvunjiika kwa iliyokuwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977.
*Mei 14, 1984: Mabondia Nassor Michael na Juma Bugingo wa Tanzania
wanashinda medali za Dhahabu katika michezo ya 36 ya Ulimwengu ya
Majeshi katika Kiwanja cha Kikundu jijini Jinja, Uganda.
*Mei 14,1941: Wayahudi 3, 600 wanakamatwa na utawala wa NAZI chini ya
Adolf Hitler wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
*Mei 14,1944: Dikteta Adolf Hitler ananusurika kuuawa katika jaribio
lililofanywa na majenerali Rommel, Speidel na Stulpnagel.
*Mei 14,1991: Robert M. Gates anakuwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi la
Marekani (CIA)
*Mei 14,1969: Cate Blanchett, mcheza sinema mashuhuri wa kie wa
Marekani aliyeshinda tuzo ya Academy katika filamu ya 'The Aviator',
anazaliwa.
*Mei 14, 1969: Canada inaruhusu utoaji mimba na matumizi ya vidonge
vya kuzuia mimba.

No comments:

Post a Comment