Monday, February 27, 2012

APRILI 21 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Aprili 21, 1964: Harold Schneider, mtafiti maarufu wa makabila ya
Tanganyika, anakamilisha ripoti yake kuhusiana na utafiti alioufanya
katioka jamii ya Wanyaturu wa Tanzania na pia mifumo ya kiuchumi ya
makabila ya Afrika Mashariki.
*Aprili 21, 1984: FAO, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa, linaelezea hatari ya kuzidi kuharibika kwa mazingira na
athari zake katika upatikanaji chakula unaohusiana na matumizi ya
nishati ya mkaa katika ukanda wa Kati wa nusu-jangwa wa Tanzania.
*Aprili 21, 1984: Kituo maarufu cha Udhibiti wa Magonjwa cha Atlanta,
Marekani (CDC) kinatoa moja ya taarifa za awali kuhusiana na ugonjwa
hatari wa UKIMWI baada ya kueleza kuwa kirusi kilichoonekana kwa
mgonjwa huko Ufaransa, kinadhjoofisha nguvu za asili za mwili
kujikinga na maradhi.
*Aprili 21, 1926: Malkia Elizabeth II wa Uingereza, anazaliwa.
1828: Noah Webster, anachapisha moja ya kamusi za kwanza na muhimu
zaidi katika historia ya lugha duniani.
* Aprili 21, 1982: Dk. Michael E. Bakey wa Houston, Texas, Marekani
anafanikisha oparesheni ya kwanza kabisa ya moyo bandia kwa binadamu.
*Aprili 21, 1729: 1729: Catherine the Great. Mtawala maarufu wa zamani
wa Urusi na mmoja wa wanawake wenye nguvu zaidi kuliko wote waliowahi
kuishi duniani, anazaliwa.

No comments:

Post a Comment