*Aprili 15, 1959: Serikali ya kikoloni nchini Tanganyika inatangaza
itatumia kila namna kuitekeleza Sheria Mpya ya kulinda misitu ya
Tanganyika ambayo ndiyo kwanza inapitishwa na Baraza la Kutunga Sheria
la Tanganyika.
*Aprili 15, 1973: Profesa James wa Chuo Kikuu cha Dare s Salaam pamoja
na Mhadhiri wa Sheria chuoni hapo, Gamaliel Mgongo Fimbo (baadaye
Profesa Fimbo) wanamaliza kuandika kitabu maarufu na muhimu kuliko
vyuote katika Sheria za Ardhi na Mila za Tanzania. Kinaitwa Customary
Land Law of Tanzania: A Source Book.
*Aprili 15, 1964: Haini Ian Smith wa Rhodesia anajitangaza kuwa waziri
Mkuu wan chi hiyo inayoitwa Zimbabwe kwa sasa.
*Aprili 15, 1452: Leonardo da Vinci, mwanafalsafa, mwanasayansi,
mchoraji maarufu na binadamu aliyejaliwa vipaji vingi anazaliwa.
*Aprili 15, 1974: Rais Diori Hamani wa Niger anaondolewa madarakani
katika mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
*Aprili 15, 1986: Marekani inaipiga mabomu Libya baada ya nchi hiyo
kutuhumiwa kuhusika na ugaidi wa ulipuaji wa ukumbi wa dansi wa La
Belle, Berlin, Ujerumani.
*Aprili 15, 1989: Watu 95 wanakufa katika ghasia ndani ya uwanja wa
mpira wa Sheffield, Uingereza.
*Aprili 15, 1978: watu 43 wanakufa baada ya teeni mbili kugongana uso
kwa uso huko Bologne, Ulaya.
*Aprili 15, 1978: Uingereza inafanikiwa kufanya jaribio la bomu la nyuklia.
*Aprili 15, 1981: Janet Cooke, mwanamke aliyeandika mkasa wa kutumia
madawa hatari ya heroine kwa miaka minane kabla ya kuachana nayo
anatoboa siri kuiwa mkasa huo uliompa uimaarufu mkubwa duniani hadi
kushinda tuzo ya heshima ya uandishi ya Pulitzer ambayo ni ya juu
zaidi duniani ilikuwa ni magirini tu. Anavuliwa tuzo hiyo.
1962: Deni la tauifa la Marekani linafikia dola bilioni 300.
No comments:
Post a Comment