*Aprili 29, 1968: Bi. Mwatumu Jasmine Mtengeti anakuwa Mtanzania wa
kwanza wa kike kuhitimu Shahada ya Sayansi (B.Sc.) kutoka Chuo Kikuu
cha New Zeland alikopata skolashipu ya Jumuiya ya Madola. Katika
Shahada hiyo alijikita zaidi katika somo la Jiografia.
*Aprili 29, 1969: Mahakama ya Rufaa ya Afrika ya Mashariki inatoa
uamuzi muhimu katika Rufaa ya Mawji Dhidi ya Arusha General Stores kwa
kueleza kuwa katika hali ya kawaida tafsiri ya Sheria ya Bunge
inayotumiwa na mahakam ni ile ya msamiati wa kawaida ki-kamusi lakini
kuna wakati misingi ya haki inalazimisha kufuatwa kwa kanuni
nyinginezo za kutafisiri zaidi tu ya lugha inayotumika waziwazi.
*Aprili 29, 1429: Joan of Arc, manamke anayeyajwa shujaa zaidi kijeshi
kuliko wote waliopata kusihi, anayaongoza majeshi ya Ufaransa na
kushinda vita vikali dhidi ya waingereza.
*Aprili 29, 1991: Watu zaidi ya 139,000 wanakufa na wengine milioni 10
kupteza makazi kutokana na kimbunga kikali huko Bangladesh.
*Aprili 29,1992: Ghasia za wamarekani weusi zinaikumba Los Angeles,
Marekani baada ya mahakama kuwaachia huru askari weupe waliompiga
isivyo halaliMmarekani mweusi Rodney King.
*Aprili 29,1991: Croatia inatangaza uhuru wake.
*Aprili 29, 1994: Israel na Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO)
wanasaini mkataba wa kushirikiana kiuchumi.
*Aprili 29,1992: Garth Brooks ananyakua tuzo katika Tamasha la 27 la
Muziki maarufu wa Marekani wa Country.
*Aprili 29,1986: 800,000 books destroyed by fire in Los Angeles Central Library
*Aprili 29,1967: Aretha Franklin, mwanamuziki maarufu mweusi wa ike wa
Marekani, anatoa albamu yake ya "Respect" inayokuja kumpatia umaarufu
mkubwa.
*Aprili 29,1970: Uma Thurman, mcheza filamu maarufu wa kike wa
Marekani, anazaliwa.
*Aprili 29,1970: Andre Agassi, mchezaji bingwa wa tennis aliyetamba
Marekani na dunia nzima, anazaliwa.
No comments:
Post a Comment