Monday, February 27, 2012

MEI 20 MATUKIO KATIKA HISTORIA

May 20
*Mei 20, 1987: Mwalimu Nyerere anakataa matumizi ya neno ‘Mheshimiwa’
kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote. Alitoa msimamo huu huko Iringa
katika mkutano wa hadhara alipokuwa akijibu swali la Kada wa CCM
Edward Matipa aliyeuliza kuhusiana na jambo hilo baada ya Bunge mjini
Dodoma kupitisha Azimio la kuwatambulisha Wabunge kama ‘waheshimiwa’.
*Mei 20, 2010: Wanasayansi katika Taasisi ya kimataifa ya Craig J.
Venter wanatangaza kuwa wametengeneza chembe hai za kwanza kabisa
kutengenezwa nje ya mfumo wa viumbe-hai asili.
*Mei 20, 1991: Michael Jordan, mchezaji maarufu zaidi wa mpira wa
vikapu duniani katika historia anatangazwa mchezaji mwenye thamani
zaidi katika mchezo huo, katika ligi maarufu ya NBA.
*Mei 20, 1293: Watu 30,000 wanakufa katika tetemeko la ardhi huko
Kamakura, Japan.
*Mei 20, 526 (mwaka mia tano ishirini na sita baada ya Kristo): Watu
250,000 wanakufa katika tetemeko huko Antiokia (sasa Syria).
*Mei 20,1992: Mwimbaji Rebel XD wa Marekani anaweka rekodi ya kuimba
kasi zaidi wa kufoka (muziki wa rap) alipoimba silabi 597 chini ya
sekunde 60.
*Mei 20,1980: Wazee 157 wanakufa baada ya nyumba ya kuhudumia wazee
waliyoishi kuungua moto.

No comments:

Post a Comment