*Aprili 18, 1960: Fabian Ngalaiswa anajitokeza kuwa mgombea binafsi
katika uchaguzi Mkuu wa 1960. Alishinda jimboni mwake baada ya TANU
kukosa kusimamisha mgombea.
*Aprili 18, 1999: Wanachama 250 waliokataliwa uanachama na chama cha
NCCR-Mageuzi wakati mgogoro ukifukuta chamani humo, wanawasilisha
malalamiko kuhusiana na hatua hiyo.
*Aprili 18, 1946: Iliyokuwa Jumuiya ya Mataifa (Chimbuko la Umoja wa
Mataifa) inavunjika.
*Aprili 18,1956: Israeli na Misri zinaingia makubaliano ya amani baina yao.
*Aprili 18,1973: Haile Gebresleassie, M-Ethiopia,alivuma sana kwa
kukimbia kasi ya ajabu na mshindi wa dhahabu katika Olimpiki ya 1996,
anazaliwa.
*Aprili 18,1977: Alex Haley, mtunzi wa kitabu kilichozaa filamu
maarufu ya Roots kuhusu utumwa wa Weusi (waafrika) huko Marekani,
anatunukiwa tuzo ya heshima ya Pulitzer.
*Aprili 18, 1963: Conan O’ Brien, mmoja wa wachekeshaji maarufu zaidi
wa televisheni duniani anazaliwa.
*Aprili 18, 1984: America Ferrera, mcheza sinema maarufu wa kike wa
Marekani anazaliwa.
*Aprili 18,1995: Joe Montana, mcheza mpira maarufu wa Marekani, anastaafu.
No comments:
Post a Comment