Monday, February 27, 2012

APRILI 7 MATUKIO MUHIMU KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Aprili 7, 1972: Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa ASP, muasisi wa
mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa kwanza wa Zanzibar anauawa kwa
risasi.
*Aprili 7,1934: Mahatma Gandhi, mwanaharakati maarufu wa India,
anasimamisha mgomo dhidi ya wakoloni wa Kiingereza.
*Aprili 7, 1975: Victoria Adams, "Posh Spice", mwimbaji mashuhuri wa
kundi la Spice Girls la Uingereza, anazaliwa.
*Aprili 7,1978: Biblia ya zamani sana iliyochapishwa na Guttenberg
inaweka rekodi kwa kuuzwa kwa dola za Marekani milioni 2 ($2,000,000)
huko New York, Marekani.
*Aprili 7,1967: Israeli na Syria zinaingia katika vita vya kugombea mpaka.
*Aprili 7, 1990: Watu 110 wanakufa katika ajali ya pantoni huko
Norway. Wengine 30 wanakufa katika ajali tofauti ya pantoni huko Burma
*Aprili 7, 1989: Manowari ya kivita ya Urusi inazama katika bahari ya
Norway na kuua mamia ya watu.
*Aprili 7, 1978: Rais Jimmy Carter wa Marekani anasimamisha
utengenezwaji wa bomu la neutroni linalofanywa na nchi yake.
*Aprili 7, 1969: mahakama ya Rufaa ya Marekani inabatilisha sheria
inayofanya jinai mtu kuwa na machapisho ya ngono.

No comments:

Post a Comment