Monday, February 27, 2012

APRILI 23 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Aprili 23, 1958: Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki (Tanganyika na
Zanzibar zikijumuishwa wakati huu) inatia hukumu muhimu katika kesi
maarufu ya Kibangeny Arap Kolil Dhidi ya Jamhuri kwa kutamka kuwa
ushahidi wa mtoto mahakamani hauwezi kukubalika mpaka ihakikishwe
kwamba mahakama iliyosikila shauri husika linawajibika ipasavyo
kuhakikisha kuwa mtoto anayetoa ushahidi anaelewa maana ya kiapo
anachokila mahakamani kabla ya kutoa ushahidi wake.
*Aprili 23, 1984: Kirusi (virus) kinachosababisha ugonjwa wa UKIMWI
(kimombo AIDS) kinatambulishwa rasmi kwa jina la HIV.
*Aprili 23, 1985: Kampuni ya Coca-Cola ya Atlanta, Georgia
inabadilisha kwa mara ya kwanza kanuni (formula) na ladha (flavour) ya
kinywaji cha Coca-Cola ambacho ndicho maarufu zaidi duniani na ambacho
pia kanuni yake ya utengenezaji (formula) ndicho kitu cha siri zaidi
katika utengenezaji bidhaa.
*Aprili 23, 1891: Wayahudi wanafukuzwa kutoko Urusi.
*Aprili 23, 1858: Max Planck, mwanafizikia maarufu sana kutoka
Ujerumani aliyeshinda tuzo ya Nobel katika Fizikia mwaka 1918,
anaaliwa.
*Aprili 23, 1897: Lester Bowles Pearson, Waziri Mkuu wa 14 wa Canada
aliyeshinda pia tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1957, anazaliwa.
*Aprili 23,
1791: James Buchanan, Rais wa 15 wa Marekani (1857-61) anazaliwa.

No comments:

Post a Comment