Monday, February 27, 2012

APRILI 28 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

* Aprili 28, 1998: Joseph Chombo, Katibu wa Chama cha kupigania haki
za Waafrika wa Tanganyika (TAAA) hukoMwanza na anayesifika kwa
kukieneza chama hichokilichokuja kuzaa TANU huko kanda ya ziwa
anaandika barua kwa wakazi na viongozi wa kiafrika wa chama cha TAA
Biharamulo, Bukoba, Missungwi (Mwanza), Musoma, Ngara na Ngudu
(Kwimba) barua inayoelezwa ilihamasisha kwa kiasi kikubwa mwamko wa
Waafrika dhidi ya ukoloni.
* Aprili 28, 1998: Tuhuma za ubadhirifu mkubwa zinaizonga menejimenti
ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
* Aprili 28, 1969: Charles de Gaulle anajiuzulu kama Rais wa Ufaransa.
* Aprili 28, 1967:Muhammad Ali, bingwa wa ngumi za uzito wa juu
duniani anakataa kujiunga na jeshi la Marekani kwenda kupigana vita
Vietnam na anavuliwa ubingwa wake kwa jambo hilo.
* Aprili 28, 1950: Jay Leno, mmoja wa wachekeshaji maarufu na matajiri
zaidi wa televisheni, anazaliwa.
* Aprili 28, 1981: Jessica Alba, mcheza filamu maarufu wa Marekani, anazaliwa.
*Aprili 28, 585 (mwaka mia tano themanini na tano): Vita maarufu kati
ya Lydia na Media vinamalizwa na kupatwa kwa jua.
Quick Reply

No comments:

Post a Comment