Monday, February 27, 2012

APRILI 13 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI

*Aprili 13, 2000: Padri Felician Nkwera anasisitiza kuendelea kwa
ibada za Kanisa lake la Wanaombi.
*Aprili 13, 2000: Kanisa la KKKT linagubikwa na migogoro.

*Aprili 13,1743: Thomas Jefferson, Rais wa 3 wa Marekani na mmoja wa
binadamu waliochangia zaidi maendeleo ya Katiba na Demokrasia duniani,
anazaliwa. Anatajwa mara nyingi pia kuwa na akili nyingi kuliko
walizonazo binadamu wengi wa kawaida.

*Aprili 13,1961: Umoja wa Mataifa unapitisha Azimio la Kulaani siasa
za Ubaguzi wa Rangi za Makaburu wa Afrika ya Kusini.

*Aprili 13,1960: Ufaransa inakuwa nchi ya nne kuthibitika kuwa na bomu
hatari la Nyuklia baada ya kufanya jaribio la bomu kama hilo katika
jangwa la Sahara barani Afrika.

*Aprili 13,1959: Vatican, Makao makuu ya Kanisa Katoliki Duniani na
makazi ya Papa (kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani), yanatoa waraka
wa kupiga marufuku Wakatoliki kuwapigia kura Wakomunisti.

*Aprili 13,1980: Marekani inayagomea mashindano ya Olimpiki ya Joto
(Summer Olympics) yaliyofanyika Moscow, Urusi. Urusi na Marekani
wakati huu ni maadui wakubwa na mataifa haya yako katika Vita Baridi.

*Aprili 13,1975: Mapinduzi ya kijeshi yanafanyika nchini Chad ambapo
Jenerali Odingar anatwaa madaraka ya nchi.

*Aprili 13,1918: Watu 38, wengi wao wagonjwa wa akili, wanakufa baada
ya moto uliosababishwa na hitilafu za umeme kuunguza hospitali ya
wagonjwa wa akili huko Oklahoma, Marekani.

No comments:

Post a Comment