Monday, February 27, 2012

APRILI 22 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*April 22, 1964: Mwalimu Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abed Amani
Karume wa Zanzibar wanaingia rasmi mkataba wa Muungano unaokuja kuzaa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku nne baadaye (Aprili 26, 1964).
*April 22,1891: Hans Meyer, mzungu wa kwanza kuupanda Mlima
Kilimanjaro, anachapisha utafiti wake kuhusiana na uzuri wa theluji
iliyoko kileleni Kibo, sehemu ya mlima huu. Chapisho lake linabeba
jina Across East African Glaciers.
*April 22, 1994: Watutsi wapato 7,000 wanauawa kinyama katika uwanja
wa michezo wa Kibuye huko Rwanda wakati wa mauaji ya kutisha na ya
kusitisha ya Kimbari ya mwaka huo.
*April 22, 1987: Maelfu ya watu wanauawa baada ya ndege za kijeshi za
Sri Lanka kurusha makombora katika maeneo waliyoishi waasi wa Tamil
Tigers.
*April 22, 1870: Vladmir Lenin, mwanamapinduzi aliyeongoza Mapinduzi
Makuu ya Urusi ya Oktoba 1917 na kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo na
pia kuukuza na kuusambaza Ukomunisti na Ujamaa kote duniani,
anazaliwa.
*April 22, 1944: Adolf Hitler wa Ujerumani na Benito Musolini wa
Italia, madikteta wawili waliouingiza Ulimwengu katika Vita Vya Pili
vya Dunia (1939-1945) wanakutana kujadili cha kufanya wakati
wanaonekana kuelemewa na majeshi ya Marekani, Urusi, Uingereza,
Ufaransa na washirika wengine.
*April 22, 1940: J. Robert Oppenheimer, Mmarekani aliyeongoza mradi
maarufu (maarufu kama Manhattan Project) uliotengeneza bomu la kwanza
la Atomiki, anazaliwa.
*April 22, 1977: Simon Peres anakuwa Waziri Mkuu wa Israeli.
*April 22, 2000: Elian Gonzales, mvulana wa Ki-Cuba aliyezua tafrani
ya ki-diplomasia na Uhamiaji alipoingia Marekani kinyemela na
kugombewa na ndugu zake anatwaliwa Katika oparesheni ya ghafla na ya
Kasi ya makachero wa FBI ili arudishwe kwao Cuba.

No comments:

Post a Comment