Monday, February 27, 2012

APRILI 26 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Aprili 26, 1964: Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa) inazaliwa rasmi
baada ya zilizokuwa Jamhuri za Tanganyika na Zanzbar kuungana na kuwa
nchi moja sasa.
*Aprili 26, 1981: Uporaji mkubwa zaidi wa fedha za benki Marekani
unafanyika katika benki moja huko Tucson, Arizona ambapo dola milioni
33 zinaibwa.
*Aprili 26, 1900: Watu 126 wanafariki huko China katika tetemeko la ardhi.
*Aprili 26, 1564: William Shakespeare, mtunzi mashuhuri wa Uingereza
na mshairi maarufu zaidi kuliko wote waliopata kuishi,
anazaliwa.Kitabu chake Merchant of Venice kilitafsiriwa na hayati
Mwalimu Nyerere aliyekipa jina la ‘Mabepari wa Venice’.
*Aprili 26, 1711: David Hume, mwanafsalsa maarufu duniani hadi leo, anazaliwa.
*Aprili 26, 1900: Charles Richter, mtafiti maarufu wa matetemeko ya
ardhi anazaliwa huko Ohio. Kipimo maarufu cha matetemeko ya ardhi
(Ritcher Scale) kinatokana na jina lake.
*Aprili 26, 1785: John James Audubon, binadamu aliyetumia muda mwingi
zaidi kuwayizama na kuwajali ndege anazaliwa huko Haiti. Leo hii jina
lake limehusishwa sana na maeneo maalum ya kutunzia viumbe asili kama
ndege.
*Aprili 26, 1914: James William Rouse, mbunifu, mwanzilishi na na
mjenzi maarufu wa mkusanyiko wa maduka makubwa mahali pamoja (Shopping
malls) anazaliwa huko Marekani. Mfano wa ‘malls’ (chanzo cha ubunifu
wake) ni kama ilivyojengwa Mlimani City Shopping Mall ya Dar es
Salaaam.
*Aprili 26, 1898: Vicente Aleixandre,mshindi wa tuzo ya Nobel katika
Fasihi mwaka 1977 anazaliwa.

No comments:

Post a Comment