Monday, February 27, 2012

MEI 17 MATUKIO KATIKA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI KOTE

*Mei 17, 1984: Benki Kuu ya Tanzania inaungua moto huku watendaji wote
wakuu wakiwa nje mbali na ofisi. Wakati ikungua Gavana Charles Nyirabu
alikuwa Mwanza, Naibu Gavana Bob Makani alikuwa Ulaya na Waziri wa
Fedha Cleopa Msuya alikuwa Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM.
*Mei 17, 1996: Alicia Machado, mrembo wa Venezuela anatawazwa kuwa
mrembo bora duniani. Ni mmoja wa warembo walioandikwa na kupigwa picha
nyingi zaidi duniani.
*Mei 17, 1986: Rajiv Gandhi, Waziri Mkuu wa India na mkewe, Sonia,
wanawasili Dar es Salaam kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini
Tanzania.
*Mei 17, 1964: Stephen Moshi anatawazwa Askofu wa kwanza wa Kanisa la
Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT)
*Mei 17, 1983: Israeli na Lebanon zinasaini mkataba wa amani.
*Mei 17, 1994: Bakili Muluzi na chama chake cha UDF wanashinda
uchaguzi mkuu wa Malawi.
*Mei 17, 1976: maelfu ya watu wanakufa katika tetemeko la ardhi huko
Uzbekhistan.

No comments:

Post a Comment