• Aprili 9, 1909: Dk. F. Stuhlmann, mtafiti na Mkurugenzi wa kwanza wa
kituo cha utafiti cha kilimo cha Amani, Tanga anachapisha matokeo
muhimu ya uchunguzi alioufanya muda mrefu kuhusiana na uingizwa wa
mazao ya chakula kutoka kwingineko katika nchi za Afrika Mashariki na
pia athari zake kiuchumi.
• Aprili 9, 1967: Jaji Saidi wa Mahakama Kuu ya Tanzania antaoa uamuzi
muhimu katika kesi ihusianayo na urithishaji ardhi kimila katika jamii
ya Wachagga ambapo analiongelea kwa kina suala la unyanyasaji wa
kijinsia unaofanywa kwa mwanamke katika masuala ya mirathi.
• Aprili 9, 1953: Jomo Kenyatta, mpigania uhuru mashuhuru wa Kenya,
anafungwa na wakoloni wa Uingereza aishi gerezani kwa miaka saba.
• Aprili 9, 1992: John Majors anachaguliwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
• Aprili 9, 1992: Manuel Noriega, Rais wa zamani wa Nicaragua anatiwa
hatini na mahakama ya Marekani kwa kupatikana na makosa ya biashara ya
madawa ya kulevya.
• Aprili 9, 1989: Mike Tyson, bingwa wa ndondi za uzito wa juu duniani
wakati huu anampiga mkatisha tiketi katika sehemu ya maegesho ya magai
pale anapoambiwa aliegeshe gari lake vizuri.
• Aprili 9, 1968: Martin Luther King., Jr. mwanaharakati mashuhuri wa
haki za weusi huko Marekani anazikwa.
• 1963: Hayati Sir Winston Churchill, Waziri Mkuu wa zamani wa
Uingereza anapewa na Marekani uraia wa chi hiyo ikiwa ni heshima ya
kwanza kabisa kutolewa na Marekani kwa binadamu aliyekwishafariki
tayari.
• Aprili 9, 1965: India na Pakistan zinaingia katika vita kugombea
mpaka wa nchi hizo.
• Aprili 9, 2005: Prince Charles,mwana wa mfalme wa Uingereza na mume
wa zamani wa hayati Princess Diana, anafunga ndoa na Camilla Parker
Bowles.
No comments:
Post a Comment