Tuesday, February 28, 2012

MARCH 22 EVENTS IN HISTORY (MACHI 22 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI)

Machi 22, 1984: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anawataka viongozi wa
Tanzania wasichoke kujiendeleza ki-elimu. Anayasema hayo katika ukumbi
wa mikutano wa Chio cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dare es
Salaam.
*Machi 22, 1973: Tanzania inaelezea wasiwasi kuhusiana na mwenendo wa
vitendo vya kibabe vya Dikteta Idi Amin wa Uganda.

*Machi 22, 1934: Watu 1,500 wanakufa na wengine 1,000 kujeruhiwa baada
ya moto mbaya kutokea huko Hakodate Japan.

*Machi 22, 1457: Biblia ya Gutenberg inakuwa ndiyo kitabu cha kwanza
kuchapishwa duniani.

*Machi 22, 1966: Yahya Ayyash, mtengenezaji mabomu hatari wa kundi la
kigaidi la Hamas maarufu kama ‘Injinia’ anazaliwa. Amehusika na vifo
vya zaidi ya Wayahudi 90 na ndiye gaidi anayetafutwa zaidi na serikali
ya Israeli.

*Machi 22, 1976: Reese Witherspoon, mcheza sinema maarufu wa Marekani anazaliwa.

*Machi 22, 1922: Mahatma Gandhi, mpigania haki maarufu wa India na
dunia nzima, anahukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na serikali ya
Wakoloni wa Uingereza.

*Machi 22, 1967: Muhammad Ali anamtwanga kwa KO bondia Zora Folley
katika pambano la kumtafuta bingwa wa ndondi duniani.
*Machi 22, 1972: Kareem Abdul-Jabbar anatangazwa kuwa mchezaji bora
zaidi wa ligi ya Kikapu ya Marekani, NBA MVP.

*Machi 22, 1963: Kashfa maarufu ya ngono ilioyomkumba John Profumo,
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza inachukua sura mpya baada ya
Profumo kudai hakuwahi kufanya mapenzi na msichana Christine Keeler.


*Machi 22, 1977: Indira Gandhi anajiuzulu U-Waziri Mkuu wa India.
*Machi 22, 1924: Allen Harold Neuharth, mwanzilishi wa gazeti maarufu
la USA TODAY, anazaliwa.

No comments:

Post a Comment