Machi 18 HISTORIA
* Machi 18, 1994: Waziri Mkuu John Malecela anayaonya magazeti ya
Tanzania kuachana na lugha isiyofaa.
* Machi 18, 1994: Benki ya Meridian Biao ambayo ilikuja kufilisika
baadaye hapa Tanzania, inatangaza kuwa ya kwanza kuleta huduma za
utoaji fedha kupitia kadi za mkopo za plasstiki (Credit cards)
* Machi 18, 1970: Queen Latifah, mwanamuziki na mcheza sinema
mashuhuri wa kike mweusi wa Marekani anazaliwa. Alitamba kama Khadijah
James ndani ya tamthiliya ya Living Single.
* Machi 18, 1963: Vanessa L. Williams, Mrembo bora Miss Amerika wa
kwanza mweusi mwaka 1983 anazaliwa huko Millwood, New York. Ni
mwimbaji mashuhuri pia.
* Machi 18, 1932: F. W. de Klerk, Rais wa Mwisho Kaburu wa Afrika ay
Kusini kabla ya weusi kupata Rais wao wa Kwanza (Nelson Mandela) .
Alikuwa Rais kuanzia mwaka 1989-1994.
* Machi 18,1928: Fidel V Ramos, President, Rais wa zamani wa
Phillipines, anazaliwa.
No comments:
Post a Comment