Monday, February 27, 2012

MEI 5 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Mei 5, 1981: Joseph Mungai, Waziri wa Kilimo wa Tanzania anaziasa
nchi za Afrika kushirikiana katika sekta za Kilimo na maendeleo
vijijini kama njia peke ya kuutokomeza umaskini uliozigubika nchi
hizi.
*Mei 5,1972: Abiria 115 waliokuwemo katika ndege ya Alitalia DC-8
wanakufa baada ya ndege hiyo kuanguka huko Palermo, Sicily, Italia.
*Mei 5,1818: Karl Marx, muasisi wa Ujamaa, Mchuni, mwanafalsafa na
mpigania haki za wanyonge, wakulima na wafanyakazi pengine maarufu
zaidi kuliko wote waliopata kuishi, anazaliwa. Communist Manifesto na
Das Kapital vimesomwa na mamilioni ya watu enzi na enzi.
*Mei 5,1944: Mahatma Gandhi, mpigania ukombozi na mwanaharakati
mashuhuri wa mabadiliko kwa njia ya amani huko India anatolewa kutoka
gerezani na wakoloni wa Ki-Ingereza.
*Mei 5,1945: Uholanzi na Denmark zinakombolewa kutoka ukaliaji
kimabavu na ukatili wa majeshi ya NAZI ya Ujerumani chini ya Dikteta
Adolf Hitler wakati huu ambapo Vita vya Pili vya dunia vinafikia
tamati.
*Mei 5,1998: Mahakama huko Marekani inahukumu kuwa Rais Bill Clinton
hana kinga ya kimamlaka kumfanya asitoe ushahidi katika kesi
inayomkabili ya masuala ya ngono na mfanyakazi mwanafunzi wa Ikulu ya
Marekani, Monica Lewinsky.
*Mei 5,1957: Adolf Scharf anachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Austria.

No comments:

Post a Comment