*Machi 21, 1978
*Mkoa wa Dar es Salaam unatangaza kuanza kutoa kwa vibali kwa
wafanyabishara wanaoingia na kutoka jijini ili kukabiliana na ugonjwa
wa kipindupindu ambao ulisababisha watu wasiopungua 1000 kulazwa
hospitali
*Machi 21, 1978: Askofu Abel Muzorewa, Bwana Ndabaningi Sithole na
Chifu Jeremiah Chirau wanaapishwa katika serikali ya Haini wa
Kiingereza Ian smith na kuonekana wamewasliti wapigania ukombozi
wenzao wa Rhodesia.
*Machi 21, 1990: Namibia inapata uhuru kutoka kwa Makaburu wa Afrika
ya Kusini chini ya chama cha SWAPO huku Sam Nujoma akiwa Rais.
*Machi 21, 1975: Ethiopia inamaliza atawala wa kifalme baada ya miaka
3,000 ya kuwa katika mfumo huo wa utawala.
*Machi 21, 1768: Jean-Baptiste-Joseph Fourier, mwanahisabati maarufu
duniani, anazaliwa.
*Machi 21,1999: Whoopi Goldberg anashinda tuzo ya 71 ya Oscar.
*Machi 21, 1963: Ronald Koeman, mcheza soka maarufu wa Uholanzi
aliyetamba na timu za Ajax, PSV na Barcelona anazaliwa.
No comments:
Post a Comment