Monday, February 27, 2012

MEI 7 MATUKIO MAKUBWA KATIKA HISTORIA TANZANIA NA ULIMWENGU

*Mei 7, 1981: mahakama Kuu ya tanzania inaamua kuwa si jambo jema
kisheria kwa mtu anayetumika kama mkalimani mahakamani atumike tena
kama shahidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo hiyo aliyokuwa
mkalimani. Ni katika rufaa ya Thobias Mbilinyi Ngasimula dhidi ya
Jamhuri ambapo inakubaliana na mkata rufaa na kubatilisha hukumu ya
kupatikana na hatia iliyokuwa imetolewa dhidi yake.
*Mei 7, 1993: Tume ya Taifa ya Menejimenti ya Mazingira (NEMC)
inakamilisha taarifa yake ya Mradi wa majaribio kuhusiana Uangaliaji
wa Hali ya Hewa Mijini (Urban Air Quality Monitoring Pilot Project).
*Mei 7,1915: Meli ya Lusitania inazamishwa majini na makombora ya
Wajerumani na watu 1, 198 kufa hapo wakati Vita vya Kwanza vya Dunia
vikiendelea.
*Mei 7,1888: George Eastman anasajili rasmi kisheria uvumbuzi wake wa
mashine ya kupigia picha (camera) aina ya Kodak.
*Mei 7,1355: Wayahudi 1,200 huko Toledo, Hispania wanauawa kwa amri ya
Mfalme Henry wa Trastamara.
*Mei 7,1711: David Hume, mwanafalsafa maarufu kutokl Scotland anazaliwa.
*Mei 7,1989: Raia wa Panama wanakataa kumpa mamlaka dikteta Manuel
Noriega kuwa tena Rais wa nchi hiyo.
*Mei 7,1995: Jacque Chirac anashinda uchaguzi wa Rais wa Ufaransa.
*Mei 7,1980: Josip Tito, aliyekuwa Rais wa Yugoslavia anazikwa.
*Mei 7,1956: Watu 300 wamapoteza maisha katika mapigano makali ya Oran, Algeria.

No comments:

Post a Comment