Monday, February 27, 2012

APRILI 14 MATUKIO MAKUBWA HISTORIA TANZANIA NA DUNIANI

*Aprili 14, 1984: Tanzania inazidi kuomboleza kwa huzuni kuondokewa na
Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine na taratibu za mwisho za mazishi
yake zinafanyika.
*Aprili 14, 1969: Mahakama ya Rufaa ya Atrika Mashariki inatoa
hukumumuhimu inayofafanua dhana nzima ya mtu kudai fidia katika
amsuala ya kuchafuliwa jina (defamation). Ni katika rufaa ya
Williamson Diamonds Dhidi ya Brown.
*Aprili 14, 1865: Abraham Lincoln, Rais maarufu wa Marekani
aliyechangia sana ukombozi wa weusi wa huko, anapigwa risasi na
muuaji wake John Wilkes Booth.
*Aprili 14, 1902: Marie na Pierre Curie wanafanikiwa kubainisha
uvumbuzi wa nguvu za kikemikali zilizoko katika madini ya Radium. Ni
moja ya mapinduzi makubwa zaidi kufanyika katika masuala ya Fizikia na
nyuklia.
*Aprili 14,1940: Majeshi ya nchi Washirika (Marekani, Urusi,
Uingereza, Ufaransa na nyinginezo) yanaikomboa nchi ya Norway kutoka
uvamizi wa madikteta Adolf Hitler wa Ujerumani na marafiki zake.
1969: Kimbunga kikali cha Tornado kinauharibu mji wa Dacca, Mashariki
mwa Pakistan na kuua pia watu 540.
*Aprili 14, 1907: Francois "Doc" Duvalier, dikteta wa zamani wa Haiti,
anazaliwa.
*Aprili 14, 1905: Frits Philips, Injinia maarufu wa Uholanzi na
mwanzilishi wa kampuni ya vifaa vya Umeme ya Philips, anazaliwa.
*Aprili 14,1977: Sarah Michelle Gellar, mmoja wa wacheza filamu wa
kike waliotamba zaidi duniani, anazaliwa.

No comments:

Post a Comment