Machi 19
* Machi 19, 1978:Andrew Young, Balozi wa Kwanza mweusi wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa anaondoka Marekani kuja Tanzania kwa ziara ya
kikazi.
* Machi 19, 1978: Makamu wa Rais, Aboud Jumbe anatangaza kuwa zaidi ya
wakazi 6,000 wa wilaya za Manyara, Ngorongoro na Serengeti
watahamishwa ili kulinda maliasili katika mbuga ya wanyama ya
Serengeti.
* Machi 19, 1860: William Jennings Bryan, mmoja wa waongeaji wazuri
zaidi katika historia ya ulimwengu anazaliwa.
* Machi 19, 1955: Bruce Willis mcheza sinema maarufu wa Marekani
aliyetamba katika filamu za Moonlighting na Die Hard anazaliwa.
* Machi 19, 1956: Alina Castro, binti wa Rais Fidel Casto wa Cuba anazaliwa.
* Machi 19, 1900: [Jean] Frederic Joliot-Curie, mshindi wa Tuzo ya
Nobel katika Fizikia mwaka 1935, anazaliwa.
* Machi 19, 1947: Glenn Close, mcheza sinema maarufu wa Marekani
aliyeng’ara na filamu za Big Chill na Fatal Attraction anazaliwa.
No comments:
Post a Comment