*Aprili 16, 1979: Majaji Mwakasendo, Nyalali na Kisanga wa mahakama ya
Rufaa ya Tanzania inatoa hukumu muhimu katika sheria ya mikataba ya
Tanzania kwa kuamua kwamba , japo kwa nadra sana, pale inapobidi
mkataba Fulani unaweza kubatilishwa iwapo kuna hila ama upande mmoja
wa mkataba umetumia mazingira ya kuufanya upande mwingine kuingia
mkataba huo pasipo kuelewa maana yake halisi. Ni katika Rufaa muhimu
ya Sluis Brothers (E.A) dhidi ya Mathias an Tawari Kitomari ambapo
kampuni hii ya Kidachi (Sluis) ilionekana imewarubuni wakulima wa
maharage wa Arusha kwa kutengeneza mikataba yenye lugha ngumu ya
kimombo ambayo wakulima hawa wasiosoma hawakuielewa.
*Aprili 16, 1977: Alex Haley, mbunifu wa filamu maarufu ya Roots
(mhusika maarufu akiwa Kinta Kunte) inayoonyesha historia ya utumwa
Marekani, anafanikiwa kugundua chimbuko la kijiji ambacho mambabu zake
walitokea huko Afrika Magharibi. Kijiji hicho ni Juffure nchini
Gambia.
*Aprili 16, 1964: Maharamia 9 wanafungwa jela kati ya miaka 25-30 kwa
kuhusika kwao na wizi maarufu kuliko wote kufanyika katika historia ya
dunia. Wizi huu ujulikanao kama The Great Train Robbery ulihusisha
wizi kamambe wa mamilioni ya fedha katika treni moja huko Uingereza.
*Aprili 16, 1947: Kareem Abdul-Jabbar, mchezaji mashuhuri zaidi wa
mchezo wa kikapu duniani wakati wake, anazaliwa. Alichezea timu za
Milwaukee Bucks na Los Angeles Lakers.
*Aprili 16, 1987: Michael Jordan anakuwa mchezaji wa pili baada ya
Kareem Abdul-Jabbar, katika historia kufunga pointi 3,000 katika msimu
mmoja wa mchezo wa kikapu wa ligi maarufu ya Marekani ya NBA.
*Aprili 16, 1992: Rais Najibullah wa Afghanistan anajiuzulu.
No comments:
Post a Comment