*Mei 13, 1954: Richard Hindorf, Mjerumani aliyeingiza zao la mkonge
nchini Tanganyika mnamo mwaka 1893, anazikwa.
*Mei 13, 1984: Marais Milton Obote wa Uganda na Daniel Arap Moi wa
Kenya wanawasili mjini Arusha kujadili namna ya ushirikiano mpya baina
yao baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka
1977.
*Mei 13,1968: Wafaransa wapatao milioni 1 (1,000,000) wanaandamana
dhidi ya utawala wa Charles De Gaulle na Pompidou.
*Mei 13,1943: Majeshi ya Ujerumani na yale ya Italia yanasalimu amri
barani Afrika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
*Mei 13,535: Mtakatifu Agapitus I anaanza utawala wake kama Papa wa
Kanisa Katoliki.
*Mei 13,1991: Winnie Mandela, mwanaharakati na mke wa zamani wa Nelson
Mandela anapatikana na hatia ya utekaji nyara watoto wanne.
*Mei 13,1857: Ronald Ross, aliyeshinda tuzo ya Nobel mwaka 1902
katika masuala ya Tiba, anazaliwa Uingereza.
*Mei 13,1729: Henry William, mtengenezaji wa mwanzoni wa vioo
viwandani, anazaliwa.
*Mei 13,1856: Peter Henry Emerson, mtu aliyeongoza kampeni za
kuibadilisha upigaji picha kuwa taaluma inayojitegemea anazaliwa.
No comments:
Post a Comment