Wednesday, February 22, 2012

AGOSTI 8 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

*Agosti 8, 1990: Irak inaitwaa na kuitangaza Falme ya Kuwait kuwa ni
sehemu na jimbo lake la 18., kwa mujibu wa utawala wa Dikteta Saddam
Hussein, aliyekuwa mtawala wa Irak.
*Agosti 8, 1988: Angola, Cuba na Afrika ya Kusini zinasaini mkataba wa amani.
*Agosti 8, 1981: Roger Federer, mchezaji mashuhuri aliyekuwa nambari
moja duniani mwaka 201 na ambaye baadhi wanamtaja kama mcheza tenisi
bora zaii kuliko wote waliopata kusihi, anazaliwa.
*Agosti 8, 1983: Rais Rios Montt wa Guatemala anaikimbia nchi baada
ya kupinduliwa.
*Agosti 8, 1966: Uatawala wa Makaburu wa Afrika ya Kusini unaliiga
marufuku kundi maarufu la Beetles kukanyaga nchini humo baada ya
mwanamuziki John Lennon wa Beetles kutoa kauli za kumkejeli Yesu
Kristo.
*Agosti 8, 1925: Wazungu 200,000 wa Kundi hatari la kibaguzi la
Marekani la Ku Klux Klan wanaandamana kwa mara ya kwanza huko
Washington D.C. wakishinikiza kubaguliwa kwa Wamarekani weusi na wao
Ku Klux kutodhibitiwa kwa msimamo wao huo.

No comments:

Post a Comment