*Agosti 1, 1980: Sheria ya kuanzishwa kwa Makumbusho ya Taifa ya
Tanzania inaanza rasmi kazi.
*Agosti 1, 1964: Chuo cha Ushirika Moshi kinaanzishwa kwa mujibu wa Sheria
*Agosti 1, 1980: Taasisi ya Utafiti wa Misitu inaanza rasmi kazi kisheria
*Agosti 1, 1968: Watu 12,000 wanakufa na majengo 60,000 yanaelezwa
kuharibika kabisa katika tetemeko kubw la ardhi nchini Iran.
*Agosti 1, 1976: Nwankwo Kanu, mchezaji wa kimataifa wa soka wa
Nigeria anazaliwa huko Owerri, Nigeria. Alikuja kuwa balozi wa UNICEF.
*Agosti 1, 1963: Coolio, mwanamuziki mweusi wa Marekani aliyetamba
sana na kibao Gangsta's Paradise mwaka 1995 anazaliwa.
*Agosti 1, 2004: George W. Bush anatangazwa kuwa amepitishwa rasmi na
chama cha Republican kugombea Urais wa Marekani. Alikuja kushinda
tena dhidi ya John Kerry wa Democrat.
*Agosti 1, 2010: Watu 900 inaelezwa kuwa walikufa katika mafuriko
huko Pakistan.
No comments:
Post a Comment