*Agosti 2, 1962: Saidi Makutika anakuwa Kamishina wa Kwanza wa Kazi
mzawa Tanganyika.
*Agosti 2, 1945: Mkataba maarufu wa kumaliza Vita vya Pili vya Dunia
wa Potsdam unamalizika baada ya kuwakutanisha Marais Josef Stalin wa
Urusi, Harry Truman wa Marekani na Waziri Mkuu Sir Winston Churchill
wa Uingereza.
*Agosti 2, 1950: Lance Ito, Jaji aliyesikiliza kesi maarufu ya O. J.
Simpson anazaliwa. Alimuachia huru kwa kumuona hana hatia O.J katika
kesi hiyo.
*Agosti 2, 1948: Dennis Prager, mwandishi wa habari na muongeaji
anayesisimua wa redio wa Marekani, anazaliwa.
*Agosti 2, 1990: Iraq inaivamia na kuikalia kimabavu Kuwait.
*Agosti 2, 1993: Watu 12 wanakufa baada ya ajali kugonga ukuta chini
ya ardhi huko Hispania.
*Agosti 2, 1994: Zaidi ya watu 120 wanakufa baada ya kutokea mlipuko
katika mgodi huko Guangxi, China.
No comments:
Post a Comment