Wednesday, February 22, 2012

AGOSTI 10 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

*Agosti 10, 1979: Mahakama ya Rufaa ya Tanzania inaanza kazi baada ya
Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, kuisaini
Sheria namba 15 ya 1979 [ndiyo pia Mabadiliko ya Kwanza ya Katiba ya
Tanzania ya mwaka 1977) iliyoianzisha kwa mujibu wa ibara ya 68A ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chombo hiki kimepewa
mamlaka ya mwisho cha kutafsiri Katiba, Sheria za nchi na kutatua
migogoro Tanzania. Mahakama hii hupokea rufaa za mahakama Kuu ya
Tanzania na ile ya Zanzibar.
*Agosti 10, 610 (mwaka wa 610 baada ya Kristo): Mtume Muhammad S.A.W
anapewa Q'uran, yaani Laylat al-Qadr, kwa mujibu wa imani ya dini ya
Uislam.
*Agosti 10,1822: watu 20, 000 wanakufa katika tetemeko kubwa la ardhi
huko Antioch (Kiswahili, Antiokia), Syria.
*Agosti 10,1960: Antonio Banderas, mcheza filamu maarufu duniani, anazaliwa.
*Agosti 10, 70: Hekalu la Pili la Israeli linachomwa moto.
*Agosti 10, 654: Papa Eugene I anaanza kuwa kiongozi wa wakatoliki
duniani baada ya Papa Martinus I.
*Agosti 10,1675: Mfalme Charles II anafungua kituo maarufu cha
Jiografia ya Hali ya Hewa cha Greenwich, mahali ulipo mstari wa kubuni
wa Greenwich unaoigawa dunia katika sehemu mbili zilizo sawa,
Mashariki na Magharibi.
*Agosti 10,1821: Missouri inakuwa jimbo la 24 la Marekani.
*Agosti 10,1833: Chicago, jiji la tatu kwa ukubwa Marekani
linaanzishwa rasmi likiwa mji mdogo wenye watu 200 tu.

No comments:

Post a Comment