*Agosti 9, 1958: Mwalimu Nyerere anaepuka kwenda jela baada ya kulipa
fainikatika kesi ya kutoa manane ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake
na wakoloni Tanganyika.
*Agosti 9, 1974: Richard Nixon anajiuzulu Urais wa Marekani kufuatia
kashfa mbaya ya Watergate. Makamu wake, Gerald Ford anakuwa Rais wa
38 wa taifa hilo kubwa duniani.
*Agosti 9, 1963: Whitney Houston, mwanamuziki maarufu wa Marekani
aliyevuma sana na kibao I will Always Love You (“Nitakupenda Daima”),
anazaliwa.
*Agosti 9, 1859: Uvumbuzi wa mashine za kupandia ngazi (elavators),
maarufu kama lift, unasajiliwa kisheria.
*Agosti 9, 1942: Mahatma Gandhi na wapigania uhuru na haki wenzake 52
India wanakamatwa.
*Agosti 9, 1841: Watu 242 wanakufa ndani ya boti kubwa walipokuwa
wakisafiri katika mto Erie, Marekani.
No comments:
Post a Comment