Wednesday, February 22, 2012

AGOSTI 15 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

*Agosi 15, 1964: Serikali YA TANZANIA inatangaza kuwa itaharakisha uelimishaji wa
Wazawa Watanzania kusimamia wenyewe mfumo wao wa sheria, zikiwa ni
siku mbili tu baada ya Augustine Saidi kuwa Jaji wa Kwanza mweusi wa
Mahakama Kuu Tanzania.
*Agosi 15, 1994: Carlos the Jackal, gaidi maarufu kuliko wote duniani
kabla ya kuibuka akina Osama Bin Laden, anakamatwa jijini Khartoum,
Sudan.
*Agosi 15, 1973: Watu watatu wanauawa na wengine 55 kujeruhiwa huko
Athens, Ugiriki, katika shambulio la kigaidi la kundi lililotisha
lililoitwa Black September .
*Agosi 15, 1947: Pakistan inapata uhuru kutoka kwa Waingereza.
*Agosi 15, 1981: Idadi kubwa zaidi ya magoli kufungwa katika historia
ya Kombe la soka la Dunia ambapo New Zelanda inaichabanga Fiji 13-0.
*Agosi 15, 1769: Napoleon Bonaparte, mtawala na Jemedari maarufu wa
zamani wa Ufaransa, anazaliwa.
*Agosi 15, 1972: Ben Affleck, mcheza sinema maarufu wa Marekani, anazaliwa.

No comments:

Post a Comment