*Agosti 16, 1986: Jaji R.B. Maganga, mmoja wa Waafrika wa mwanzo kuwa
Majaji wa Mahakam Kuu Tanganyika, anafariki dunia.
*Agosti 16, 1992: Moses Kiptanui wa Kenya anaweka rekodi ya dunia
anapokimbia umbali wa kilometa 3 (mita 3,000) kwa kutumia dakika 7,
sekunde 28 na nukta 96 tu (7:28.96)
*Agosti 16,1988: Nelson Mandela, mfungwa wa kisiasa nchini Afrika ya
Kusini anapata maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu (T.B) akiwa
gerezani.
*Agosti 16,1863: Marekani inakomesha utumwa nchini humo.
*Agosti 16,1987: Watu 156 wanakufa na mmoja kunusurika baada ya ndege
ya Northwest Airlines kuanguka huko Detroit, Marekani.
*Agosti 16,1985: Madonna, mwimbaji maarufu wa Marekani, anafunga ndoa
na mcheza filamu Sean Penn, siku ambayo Madonna alitimiza miaka 27
tangu azaliwe.
No comments:
Post a Comment