*Agosti 22, 1984: Hali ya upepo wa kisiasa Zanzibar inaelezwa kuchafuka.
*Agosti 22, 1902: Rais Teddy Roosevelt wa Marekani anakuwa kiongozi wa
kwanza duniani kupanda gari. Ni muda mfupi baada yagari la kwanza
duniani kutengezwa na Henry Ford.
*Agosti 22, 1987: Madonna, mwanamuziki machachari wa Marekani anavuma
kwa sifa baada ya wimbo wake "Who's That Girl” (Nani msichana Yule?)
kutamba katika chati za muziki Marekani na duniani kote kwa kushika
nambari 1.
*Agosti 22, 1994: Ushahidi wa vinasaba (DNA) unaonyesha kuwa O. J.
Simpson alimuua aliyekuwa mkewe, Nicole Simpson na mumewe mpya, Ron
Goldman. Kesi ya Simpson ndiyo inayotajwa kuwa moja ya zilizo maarufu
zaidi katika kesi za jinai za karne iliyopita.
*Agosti 22, 1911: Kazi ya sanaa ya uchoraji maarufu na ya thamani
zaidi, ile ya Mona Lisa, inaporwa kutoka ilipohifadhiwa. Ilipatikana
miaka miwili baadaye.
*Agosti 22, 1984: Rais Ronald Reagan na makamu wake, George Herbert
Bush (Bush mkubwa) wanapitishwa tena kugombea Urais na Umakamu Rais wa
Marekani kupitia chama cha Republican.
*Agosti 22, 1982: Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon anawaomba
Waplaestina wajadili kuishi pamoja na Wayahudi kwa amani.
No comments:
Post a Comment