Wednesday, February 22, 2012

JULAI 30 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

Julai 30 Historia
*Julai 30, 1960: Marko Mihayo anawekwa wakfu kuwa Askofu wa kwanza
Mtanzania wa Kanisa Katoliki jimbo la Tabora.
*Julai 30, 1997: Watu 14 wanauawa katika mabomu mawili ya kujitoa
muhanga huko Jerusalemu, Israeli.
*Julai 30, 1990: Waumini kati ya 200-600 wanauawa jijini Monrovia,
Liberia baada ya askari kulivamia kanisa na kuanza kumimina risasi.
*Julai 30, 1974: Hilary Swank, mcheza sinema maarufu wa kike wa
Marekani, anazaliwa.
*Julai 30, 1947: Arnold Schwarzenegger, Gavana wa jimbo tajiri la
California (Marekani), mtunisha misuli na mcheza sinema mashuhuri
aliyetamba na filamu kama Commando na Terminator, anazaliwa huko
Austria. Baadaye alikuja kuwa raia wa Marekani.
*Julai 30, 1971: Watu 162 wanakufa baada ya ndege aina ya Boeing 727
ya Japan kuanguka inapogongana na ndege ya kutungulia ndege nyingine,
aina ya F-86.
*Julai 30, 1980: Vanuatu inapata uhuru wake kutoka kwa Wafaransa na
Waingereza waliotawala pamoja.
*Julai 30, 1988: Mfalme Hussein wa Jordan analiacha huru eneo la
ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na ambalo sasa linakuwa chini ya
himaya ya Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO)
*Julai 30, 1988: Ronald J. Dossenbach anaanza kuiendesha baiskeli yake
kwa muda wa siku 13, masaa 15 na dakika 4 mfululizo na kuweka rekodi
ya dunia, alipoendesha baiskeli hiyo kutkea mji wa Vancouver hadi
Halifax huko Canada.

No comments:

Post a Comment