*Julai 29, 1984: Timu ya wacheza sarakasi wa kimataifa wa China
inawasili Tanzania kwa ziara ya siku 13.
*Julai 29, 1883: Benito Mussolini, Dikteta wa Italia kati ya 1922-43
na rafiki mkubwa wa Adolf Hitler wa Ujerumani, anazaliwa.
*Julai 29, 1974: Kamati ya Sheria ya Bunge la Marekani inapiga kura
kama Rais Richard Nioxon aondolewe madarakani au la.
*Julai 29, 1783: Watu 9,000 wanakufa kufuatia mlipuko wa volkano
katika mlima Skaptar, kisiwani Iceland
*Julai 29, 1986: Watu 30 wanakufa katika mlipuko wa bomu huko Beirut
Magharibi, Lebanon, Mashariki ya Kati.
*Julai 29, 1993: Mahakama ya Rufaa ya Israeli inabatilisha hukumu ya
kifo dhidi ya John Demjaujuk, ambaye alihukumiwa awali kuhusika an
ukatili wa hali ya juu hidi ya maelfu ya Wayahudi katika kambi za
mateso za Manazi wa Ujerumani.
*Julai 29, 1975: Sheya Shipanga, Miss Namibia Universe 1997, anazaliwa.
*Julai 29, 1995: Monica Seles, mchezaji mahiri wa kike wa tenisi
duniani, anarejesha tena hadhi yake anapombwaga Martina Naratilova .
*Julai 29, 2010: Abiria wote 152 waliokuwemo katika ndege ya Airblue
202 wanakufa inapoanguka katika vilima vya Margalla , karibu na
Islamabad, Pakistan.
No comments:
Post a Comment